Wednesday, August 1, 2012

BUNGE LISIZUIWE KUINGILIA MGOGORO KATI YA WALIMU NA WANAFUNZI DHIDI YA SERIKALI KWA KISINGIZIO CHA KESI KUWA MAHAKAMANI


Mbunge wa Jimbo la Ubungo, (CHADEMA), John Mnyika.
Tarehe 1 Agosti 2012 niliieleza Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia swali langu la msingi bungeni  kwamba serikali hutoa ruzuku (capitation grants) kwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari za Umma zikiwemo za Jimbo la Ubungo, japo utekelezaji wa sera husika huwa unasuasua sana kwa kiwango kilichowekwa kutokulingana na mahitaji halisi ya wanafunzi; viwango vinavyotengwa katika Bajeti ni chini ya vinavyotajwa kwenye Sera na Fedha hazitolewi zote isipokuwa hutolewa kidogo kidogo na hazifiki kikamilifu mashuleni;  nikahoji ni lini serikali itarekibisha hali hiyo ili kuboresha elimu nchini.

No comments:

Post a Comment