Misri imetumia Helicopter kufanya mashambulizi ya
mizinga dhidi ya wakereketwa wenye imani kali walio katika eneo la Sinai
tangu mwaka 1973 katika kile jeshi la Misri lililochotaja kama
shambulio la kurejesha utulivu.
Matumizi ya anga ni ishara ya mabadiliko ya vita
vya Misri dhidi ya wakereketwa wa Kiislam ambao wamezidisha shughuli
zao katika eneo lenye milima na jangwa lenye mpaka na Israili na Gaza.
Mapema
wiki hii wapiganaji wakereketwa waliishangaza Misri kwa ujasiri wao kwa
shambulizi ambamo askari 16 waliuawa, magari ya jeshi yakaibwa na
kuelekea Israel kwa lengo la kujaribu kufanya shambulio jingine.
Katika taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya
taifa jeshi limesema kua limeanzisha operesheni ya mchanganyiko wa
vikosi kwa kutaka kurejesha utulivu huko Sinai, majeshi yakiungwa mkono
na Jeshi la anga.
Shambulio la siku ya jumapili ndio baya kuwahi
kufanywa huko Sinai kwa miaka mingi na hatari kuliko yote dhidi ya
vikosi vya Misri ikiashiria ongezeko la vitendo vinavyokiukaq sheria
katika eneo hilo.

Shambulio la wakereketwa
Katika tukio la hivi karibuni, watu wenye silaha
waliwafyatulia risasi walinzi kwenye vizuizi huko El -arish, mji mkuu
wa Wilaya ya Sinai, mji ulio umballi wa kilomota 50 kutoka mpaka wa Gaza
na Israili.
Ghasia kwenye mpaka wa Israel na Misri inaweza kutishia mkataba wa amani baina ya nchi hizi mbili.
Hio ndio sababu Israel imeiambia Misri ichukue
hatua za kusuluhisha vurugu badala yake kupeleka vikosi vyake. Israel
imekubali kuondoa baadhi ya masharti yanayozuwia shughuli za kijeshi
katika Sinai ili Wa Misri waweze kuingiza vikosi zaidi.
Lakini uvamizi wa Misri dhidi ya kile
walichokiita magaidi hautobadili lolote katika sehemu ya Sinai
inayokaliwa na makabilia ya Wa Bedwini wenye fikra huria.
Ni eneo linalovutia kwa makundi ambayo
yangependa kutumia sehemu isiyokua na utaratibu wowote wa uongozi kwa
aijili ya kuifika Israili.
Rais wa Misri Mohammad Mursi aliahidi kwamba atadhibiti eneo la Sinai kwa ukamilifu.
Rais wa Misri Mohammad Mursi aliahidi kwamba atadhibiti eneo la Sinai kwa ukamilifu.
*****thanks for visiting: www.ezekiakasege.blogspot.com*****
No comments:
Post a Comment