UN YATEMBELEA VIJANA KUWAHAMASISHA KUWA WAJASIRIAMALI ILI KUPUNGUZA UMASIKINI
Bi. Harriet Macha kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) akizungumza na mtandao wa vikundi vya vijana kata ya Kibada -Kigamboni akiwaeleza jinsi Umoja wa Mataifa unavyohusika katika maendeleo ya vijana ikiwemo kuwaelimisha haki zao, kuwawezesha kujitambua na kujua umuhimu na kazi za mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini.
Naibu Mwenyekiti wa kikundi cha vijana kata ya Kibada akizungumzia changamoto zinazowakabili kama kikundi ikiwemo ukosefu wa maktaba ambazo zingewawezesha kusoma na kujua mashirika hayo yanafanyaje. Pia tatizo lingine ni jeshi la polisi kuwafikiria na sheria zake ikiwemo kuwapangia muda wa kutembea, kukithiriri kwa rushwa mambo ambayo yanachangia kuongeza uduni wa maisha ya vijana.
Mmoja wa mwanakikundi wa vijana kata ya Kibada-Kigamboni mwenye kipaji cha kuigiza akionyesha uwezo wake wa kuigiza ikiwemo jinsi vijana wanavyokwamishwa kuanzia kwenye sekta ya elimu na kujiajiri na hata hivyo Bi. Harriet Macha wa UNIC alitoa ushauri jinsi ambavyo Shirika hilo linavyofanya kazi na serikali na mipaka yake.
Mwanakikundi wa kata ya Kibada Kigamboni akielezea kipaji chake cha ususi kilichompelekea kujiajiri na kujitegemea na kuahidi kutoa mafunzo kwa wasichana wenzake.
Pichani Juu na Chini ni Bi. Harriet Macha kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) akizungumza na vijana Somangile-Kigamboni kutoka kikundi cha 'Kigamboni Peer Educator Network' (KIPENET) kuhusiana na kazi za shirika hilo na huku akipokea changamoto kutoka kwao.
Mwenyekiti wa vijana wa KIPENET Sagara Msumi akitoa tathmini ya mafanikio yao tangu waanze kufanya kazi na UN yanaonekana kufuatia kupungua kwa matukio ya mimba za utotoni kutokana na kusambaza vijarida vinavyotolewa na umoja wa Mataifa.
Wanawake wa kikundi cha 'Save The Women Tanzania' wakitoa burudani ya uigizaji wanayotumia kutoa elimu kwa jamii mbele ya mwakilishi kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (hayupo pichani).
No comments:
Post a Comment