

NI mwendo wa kumsaka staa wa kike ambaye hajaolewa mwenye mvuto kuliko wenzake. Shindano linaitwa The Ijumaa Sexiest Girl 2011-2012. Kwa kifupi kasi ya wasomaji kupiga kura ni kubwa! Mpambano ni mkali kati ya Wema Sepetu na Agnes Gerald ambapo kila mmoja amekuwa na kimuhehume cha kujua matokeo.
Mratibu wa shindano hili, Imelda Mtema amesema kura zimekuwa zikimininika kwa wingi lakini tofauti ya kura imekuwa si kubwa kiasi kwamba si rahisi hata kutabiri mshindi.
Hata hivyo, wiki hii hakuna anayetoka lakini wiki ijayo, mshindi atapatika na atajipatia zawadi kemkemu kutoka kwenye duka la vipodozi la Shear Illusions ambao ni mmoja kati ya wadhamini wa shindano hilo.
Unachotakiwa kufanya wewe msomaji ni kumpigia kura mrembo anayestahili kuibuka mshindi kwa kuandika jina lake kisha kulituma kwenda namba 0786-799120.
No comments:
Post a Comment