Monday, September 17, 2012

MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI YANAYODHAMINIWA NA AIRTEL YAANZA MKOANI IRINGA LEO


Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mbando (kushoto) akimkabidhi Modem ya Airtel 3.75G Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo ya Simu ambao ni wadhamini wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa inayofanyika mkoani Iringa. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani. Pereira Silima (wapili kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma. Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama yameanza leo kitaifa Mkoani Iringa.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, akimkabidhi cheti cha heshima kwa kuwa wachangiaji katika kampeni ya kupambana na kupunguza ajali barabarani pamoja na Wiki ya Nenda kwa Usalama kitaifa, Meneja wa Airtel Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Beda Kinunda. Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika ufunguzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa mkoani Iringa.
Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya ASAS, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Mkoa wa Iringa, Salim Ahmed, akipokea cheti cha heshima kwa kuwa wachangiaji katika kampeni ya kupambana na kupunguza ajali barabarani pamoja na Wiki ya Nenda kwa Usalama kitaifa, kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi. Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika ufunguzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa mkoani Iringa.
Kiongozi wa Kundi la Wazee Sugu, King Kikii, akiongoza waimbaji wa kundi hilo kutoa burudani ya muziki katika uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa iliyoanza jana mkoani Iringa.
Baadhi ya walemavu wakiingia uwanjani katika uwanja wa Samora mjini Iringa katika Uzinduzi wa Wiki ya kitaifa ya Nenda kwa Usalama iliyozinduliwa jana mjini hapa huku Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel ikiwa mdhamini mkuu.
----
THE CURRENT ROAD TRAFFIC CARNAGES IN THE COUNTRY CANNOT BE LEFT TO CONTINUE UNCHECKED
·         AIRTEL WOULD WANT TO SEE ROAD TRAFFIC ACCIDENTS ARE REDUCED TO ZERO,
September17: The current road traffic carnages in the country cannot be left to continue unchecked, and hence continue claiming the lives of innocent Tanzanians brutally.

The remark was given by The President of United Republic of Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete at the inaugural of the national event for the road safety week taking place in Iringa city, Iringa region.

Reading the President’s speech, the Minister for Home Affairs Emmanuel Nchimbi, who officiated the event on his behalf, said that statistics for road traffic accidents are shocking and calls for actions to end them, and this is a task for all road users, and not the traffic police only.

According to the President, between June 2008 and June 2012 a total number of 15, 499 innocent Tanzanian’s lives were cut short in avoidable road accidents.

He said out of the 15, 499 road traffic accidents; 5, 117 involved pedestrians, 4,532 (passenger), 2,414(motorcycle cyclists), 2,171(bicycle cyclists), 1,034 (drivers) and 222 (pushcart pushers).

“Despite all the efforts by police force and other stakeholders road traffic accidents at present are still not in control and hence calls for concerted efforts to address this problem,” said the President adding that this is unacceptable and should be brougyt to an end.

According to the President the statistics are shocking and calls for our concerted efforts to end these menace, everybody, every organization should have a contribution in ending this culpable accidents, while we can’t have a one answer fits all, to begin with changing the attitude of road users will be an issue of paramount importance.

Kikwete said labour force is killed or disabled, causing serious economic loss to the family and communities apart from losing their contribution in terms of labour but the education given to the deceased is lost as well, the ability to effectively contribute to the family is also lost.

“Currently road transport accounts almost 90 percent of both passenger and goods transportation, we can’t live this to chance we need proactively take actions sooner than later,” said Jackson Mmbando from Airtel Public Relations’ Manager.

“This is a legal and moral duty to us all, article three of the declaration of human rights states that “Everyone has the right to life, liberty and security of person.” no ones life should be terminated abruptly or no one should be rendered deformed or disabled. It is a moral thing to do in a sense that we have the right to protect our fellow human beings and assist them where we can. Life’s true happiness is on assisting others,” said one of the driver who attended the event and identified himself by one name only as Juma.

Juma said road traffic accidents cause a burden to the health care system, sometimes they are overwhelmed by the victims and hence fail to offer quality services to the victims

“Road traffic accidents deplete income as money which would have been used in other developmental priorities like education, food, health is relocated to vehicle maintenance,” he said.

Airtel Tanzania is the main sponsors of the event has pledged to continue supporting activities aimed at adding knowledge to stakeholders and law enforcers on the causation of road traffic accidents and what need to be done to prevent them as well as awareness raising to road users particularly children.

“Airtel would want to see road traffic accidents are reduced to zero, in this case, Airtel will be happy even if we were able to reduce the road carnage even by 1%,” said Mmbando adding that his company will continue supporting these efforts.

Salim Abri the Iringa region Road safety Council, called for road users and particularly drivers to be extra careful, with the improved roads, so that they do not become catalysts for road carnages, " Our roads are being improved, the Tanzania-Zambia highway has been improved and we are witnessing the increase in accidents," he said

The Road Safety Week begun yesterday and ends on Friday the 22 of September, the week is used to raise awareness on issues pertaining to road safety in the country
------------
HOTUBA YA MGENI RASMI KWENYE UFUNGUZI WA MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI KITAIFA MKOANI IRINGA
TAREHE 17/09/2012 
·        Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Dkt. Christine Ishengoma (MB),
·        Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Pereira Silima (MB),
·        Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na Naibu Waziri - Wizara ya Ujenzi, Mhe. Eng. Jerryson Lwenge (MB),
·        Makatibu Wakuu wa Wizara za Ujenzi na Mambo ya Ndani ya Nchi,
·        Kamishana Paul Chagonja, mwakilishi wa Inspekta Jenerali wa Polisi,
·        Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani (T),
·        Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani (M) Iringa,
·        Wageni waalikwa,
·        Wanahabari,
·        Mabibi na Mabwana,
Ndugu Wananchi,
Awali ya yote napenda kuchukua fursa hii ya kipekee kulishukuru Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kwa kunipa heshima hii kubwa ya kuwa Mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani kitaifa hapa Mkoani Iringa.
Aidha, nawashukuru ndugu zangu wa Iringa kwa mapokezi makubwa kwangu na ujumbe wangu wote. Naomba moyo huu wa upendo kwa ndugu zenu, muudumishe. Halikadhalika, nawapongeza sana kwa kujitokeza kwenu kwa wingi katika uzinduzi huu wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani, ambayo mwaka huu inaadhimishwa kitaifa hapa mkoani kwenu.
Ndugu zangu wa Iringa, ni matumaini yangu kwamba mtaitumia nafasi hii vizuri kuweza kujielimisha kupitia kwa wataalam waliopo kwenye mabanda mbalimbali hapa uwanjani kwa kuuliza maswali na kujifunza mbinu za namna ya kuziepuka ajali za barabarani.
Huu ni wasaa mwingine ambapo napenda kuwapongeza wadau wote wa usalama barabarani kwa jitihada zenu ambazo mmekuwa mkizifanya katika kupambana na ajali za barabarani. Hata hivyo, juhudi kubwa zinatakiwa kuongezwa ili hatimaye kupunguza kama sio kumaliza kabisa kero hii kubwa kwa wananchi. AJALI ZA BARABARANI ZINAZUILIKA NA HAZIKUBALIKI.
Ndugu Wananchi,
Napenda pia kuchukua nafasi hii kutoa mkono wa pole kwa ndugu na jamaa wote ambao wamepoteza wapendwa wao kutokana na ajali za barabarani, Mwenyezi Mungu awape moyo wa subira na azilaze roho za marehemu mahali pema peponi – Amin.
Lakini kwa majeruhi wote wa ajali za barabarani, na wote waliopata vilema vya kudumu. Natoa pole kwenu nyote. Mwenyezi Mungu awape nguvu na awabariki ili muweze kupona haraka na kurudi kwenye majukumu yenu ya kulijenga Taifa.     
Mabibi na Mabwana,
Makundi yote ya watumiaji wa barabara yana wajibu mkubwa yanapozitumia barabara zetu. Makundi haya ni pamoja na madereva, watembea kwa miguu, wapanda pikipiki na baiskeli, wasukuma mikokoteni, abiria n.k.  Ikumbukwe kuwa wajibu wa kuzuia ajali za barabarani ni wa kila mtumiaji wa barabara na sio wa Serikali pekee, kwani kwa pamoja tukishirikiana ajali za barabarani tutazipunguza. Wote tunawajibika katika kupambana na kuzuia ajali za barabarani. Hivyo inatubidi tushirikiane kuelekezana na  kumuonya kila mmoja wetu anapovunja sheria na kanuni za usalama barabarani.
Ndugu Wananchi,
Takwimu za ajali za barabarani zinazotolewa na Jeshi la Polisi zinaonyesha kuwa, kwa takriban miaka mitano iliyopita yaani kuanzia mwaka 2008 hadi Juni 2012,
§  Watembea kwa miguu 5,117 walifariki kutokana na ajali za barabarani;
§  Kundi hili la waathirika limefuatiwa na vifo vya abiria 4,532;
§  Wapanda pikipiki ni vifo 2,414;
§  Wapanda baiskeli waliofariki ni 2,171;
§  Madereva waliofariki ni 1,043 na
§  Wasukuma mikokoteni 222 nao walifariki katika kipindi hicho.
Kwa kipindi hicho cha miaka minne na nusu tu tumepoteza ndugu zetu 15,499 na majeruhi 87,737. Hali hii haikubaliki.
Ndugu Wananchi,
Kwa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na matukio mengi ya ajali zinazohusisha wapanda pikipiki. Mkiangalia takwimu nilizozisoma hivi punde mtaona kwa kipindi cha miaka minne na nusu jumla ya wapanda pikipiki 2,414 wamepoteza maisha kutokana na ajali za barabarani na majeruhi 14,422. Vifo hivi na majeruhi vingeweza kuepukika endapo wapanda pikipiki wangezingatia vema Sheria na Kanuni za Usalama Barabarani.
Ajali hizi zimekuwa zikichangiwa na sababu mbalimbali. Madereva wa magari na pikipiki wamekuwa ni sehemu kubwa ya vyanzo vya ajali kwa kutokuzingatia yafuatayo:
§  Kuendesha kwa mwendo kasi usioruhusiwa kisheria,
§  Kuyapita magari yaliopo mbele bila ya kuchukua tahadhari,
§  Kuendesha magari mabovu barabarani,
§  Kutoheshimu alama na ishara za barabarani,
§  Kuendesha gari au pikipiki bila leseni,
§  Kutokuvaa kofia ngumu kwa wapanda pikipiki,
§  Kubeba abiria zaidi ya mmoja kwenye pikipiki,
§  Kuendesha gari au pikipiki huku akiwa amekunywa au ametumia kilevi,
§  Kuzidisha mizigo au abiria kwenye gari,
§  Kubeba abiria kwenye magari ya mizigo,
§  Kutokujali watumiaji wengine wa barabara,
 Kupitia maadhimisho haya, nawasihi watumiaji wote wa barabara hususani madereva, abiria, wapanda pikipiki, watembea kwa miguu, wapanda baiskeli, wasukuma mikokoteni n.k. kuzingatia yafuatayo ili kuzuia ajali za barabarani.
§  Kuzingatia Sheria na Kanuni za Usalama Barabarani,
§  Kuacha kushabikia mwendokasi kwa madereva,
§  Kuhakikisha wanavuka barabara kwa kutumia vivuko vya watembea kwa miguu (zebra crossing),
§  Kuacha kuendesha baiskeli au kusukuma mikokoteni katikati ya barabara,
§  Wasiwaache watoto wadogo kutembea barabarani peke yao bila ya mlezi au mwangalizi n.k. 
Ni matumaini yangu kwamba wote tukizingatia Sheria na Kanuni za Usalama Barabarani kwa ujumla tutaondokana na ajali za barabarani.
Ndugu Wananchi, Mabibi na Mabwana,
Natoa wito wa kuhakikisha kuwa yafuatayo yanafanyika kwa nguvu na kasi zaidi ili kudhibiti ajali za barabarani. Hayo ni pamoja na:
§  Kutekeleza Azimio la Umoja wa Mataifa (UN Decade of Action for Road Safety) linalotaka nchi wanachama kupunguza vifo na majeruhi kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2020,
§  Kuanza kutumika kwa mfumo wa kuweka alama kwenye leseni za udereva (points system) ili kuwaondoa madereva wanaokithiri kwa kukiuka sheria,
§  Kurekebishwa kwa Sheria za Usalama Barabarani ili ziendane na wakati na zitilie maanani namna ya kudhibiti wimbi la ajali za barabarani,
§  Kikosi chetu cha Usalama Barabarani kiimarishwe na Jeshi la Polisi liongeze nguvu katika kudhibiti uhalifu pamoja na ajali za barabarani,
§  Tuongeze juhudi katika kutoa elimu ya kuhamasisha umma juu ya madhara ya ajali za barabarani, pamoja na kuhakikisha kuwa mafunzo kwa watendaji wote, kama askari polisi, madereva wa kila ngazi na aina, yanapewa uzito mkubwa zaidi,
§  Elimu ya Usalama Barabarani katika shule zetu za msingi, sekondari nk ipewe uzito zaidi,
§  Wamiliki wa mabasi na magari ya mizigo waelimishwe juu ya nafasi yao katika kudhibiti wimbi la ajali za barabarani,
§  Shirika la Viwango Tanzania (TBS) liongeze nguvu katika kukagua mara kwa mara viwango vya matairi, vipuri na mabodi ya mabasi nchini,
§  Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) wahakikishe kuwa barabara zinatengenezwa, kurekebishwa na kuweka alama pamoja na michoro stahiki barabarani,
§  Mfumo wa ukaguzi wa magari wa lazima (Mandatory Vehicle Inspection) uanzishwe sasa ili kuhakikisha usalama wa magari yanayotumika katika barabara zetu,
§  Kuweka mkazo katika shughuli za utafiti wa suala la usalama barabarani ili kupata suluhu ya namna ya kuzitokomeza ajali za barabarani, na
§  Suala la usalama barabarani liwe ni ya ajenda ya kitaifa pamoja na kuwahusisha kikamilifu Washirika wetu wa Maendeleo, hasa wale ambao wamepiga hatua kubwa katika maendeleo ya nyanja hii.
Mwisho:
Napenda nihitimishe kwa kuwashukuru tena wasafirishaji wote kwa kazi zao na kwamba waendelee kushirikiana na BARAZA katika kupambana na ajali za barabarani.
Aidha, ninawashukuru wadau wote na ninaomba waendelee kushirikiana na kushirikishwa katika azma hii ya mapambano dhidi ya ajali za barabarani. Daima, lengo letu liwe katika kuboresha hali ya usalama barabarani nchini. 
“PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”. 
Kwa hayo machache sasa natamka kwamba:
MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI 2012 YAMEZINDULIWA RASMI.
Ahsanteni kwa kunisikiliza.

No comments:

Post a Comment