Friday, September 28, 2012

Mtibwa: Yanga wa kawaida sana


KLABU ya Mtibwa Sugar imesema haiihofii Yanga kwa kuwa ni timu ya kawaida kama zilivyo nyingine.
Yanga na Mtibwa zinatarajiwa kuumana leo kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Akizungumza na Championi Jumatano, meneja wa timu hiyo, David Gboya, alisema Yanga ni timu ya kawaida, isipokuwa inapata sifa nyingi kupitia jina tu na siyo uwanjani.
“Yanga wa kawaida, isipokuwa jina lao ndilo lipo juu, lakini viwango vya wachezaji vipo sawa na sisi hakuna cha kusema sijui tunamuwekea ulinzi mchezaji fulani, hiyo haipo, sisi tunacheza kitimu.
“Lakini pia katika soka kuna matokeo matatu, hivyo atakayecheza vyema ndiye atakayeondoka na ushindi,” alisema Gboya.
Yanga ilitoka sare ya bila kufungana na Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine, wakati Mtibwa ililazimishwa sare kama hiyo na Polisi Moro kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

No comments:

Post a Comment