Mahojiano na Mawassi Lahcen, Casablanca
Katika eneo la wazi lililoandaliwa na mapinduzi wa chemuchemu za Uarabuni (Arab Spring), Waislamu wenye siasa kali wanaunda vikundi vipya kadhaa kusukuma mbele ajenda yao.
Wanaounga mkono brigedi ya Libya inyojiita Ansar al-Sharia wakipiga kaulimbiu za kidini wakiwa wameshikilia bendera ya washirika wa al-Qaida kupinga maandamano ya umma dhidi ya wanamgambo huko Benghazi tarehe 21 Septemba. Wakaazi wa Benghazi wanalaumu Ansar al-Sharia kwa shambulio la tarehe 11 Septemba katika ubalozi wa Marekani, [Abdullah Doma/ AFP]
Kwenye mstari wa mbele wa wimbi kubwa la Wasalafi huko Tunisia, Libya na Yemen ni vikundi vinavyokusanyika chini ya kivuli cha "Ansar al-Sharia". Kwa mara ya kwanza, wachambuzi wengi waliamini kuwa vikundi hivi vilikuwa ni jaribio la Wasalafi wa sasa kufuata hali mpya na kwamba mwishoni wataachana na itikadi ya vurugu za jihadi.
Hata hivyo, kwa kadri mtafiti wa Morocco Abdellah Rami anavyoelezea, vikundi vya Ansar al-Sharia kwa sasa vinafanya kazi kama "taswira ya itikadi, hazina ya ubinadamu na watoaji wa fedha kwa wapiganaji wa al-Qaida." Sabahi ilikaa chini na Rami, mchambuzi wa masuala ya kisiasa aliyebobea katika vikundi vya Kiislamu katika Kituo cha Sayansi Jamii cha Morocco, kujadili tukio hili jipya na matarajio yake.
Sabahi: Unachukuliaje kutokea kwa vikundi kadhaa vipya vya Wasalafi vinavyojiita Ansar al-Sharia kuwa ni kutokea tu kwa bahati au ni sehemu ya mpango mkubwa?
Abdellah Rami: Mimi silifikirii hili kama tukio la bahati tu. Hili kwa hakika ni matokeo na mipango inayodhamiria kujizoesha tena mazingira mageni ya jihadi ya Wasalafi wa sasa kwenda kwenye hali mpya ambayo imetengenezwa na mapinduzi ya Chemuchemu ya Uarabuni (Arab Spring) katika kanda hiyo.
Hili linathibitishwa na viashiria vingi, ikiwemo mikutano ambayo ilifanywa na viongozi ambao wako nyuma ya jitihada hizi, ambao ni ishara ya wanajihadi wenye historia ya jihadi huko Afghanistan na kwingineko..
Kama lilivyo jina, ninafikiri linaendana na utashi wa Osama bin Laden kabla ya kuuawa, ambapo alilitaka kundi lake kubadilisha jina la al-Qaida na kuchagua jina jipya ambalo linaendana kwa karibu na dhamira ya Waislamu. Inaonekena kuwa jina "Ansar al-Sharia" linafaa sana kwa lengo hili, na hasa ikichukuliwa asili ya alama yake na matokeo mazito katika hisia za kidini katika jamii ya Kiislamu. Kwa hivyo, jina hilo halikuchaguliwa ovyo ovyo, ila ni matokeo ya mipango na makubaliano. Lilichaguliwa kulingana na umuhimu mkubwa na alama ya jina hilo.
Hata hivyo, tunapaswa kuzingatia kuwa jina lenyewe si jipya, ikichukuliwa kuwa Abu Hamza al-Masri, ambaye kwa sasa amefungwa huko Uingereza na alikuwa anatakiwa na Yemen na Marekani kwa kuhusika katika uhalifu wa kigaidi, amekwishatoa jina hilo kwa kikundi chake ambacho alikianzisha London baada ya kurudi kutoka Afghanistani mwaka1994. Abu Hamza alikuwa anadhamiria kuifanya Ansar al-Sharia kuwa asasi ya kimataifa ikiwa na matawi katika nchi nyingi.
Kuanguka kwa kuungwa mkono al-Qaida
Sabahi: Huu ni ubadilishaji wa jina la al-Qaida, kama bin Laden alivyopendekeza, au kundi hili jipya linaashiria kusambaratika kati ya Wasalafi na mtandao wa kigaidi wa dunia?
Rami: Hapana, hakuna msambaratiko. Kwa maoni yangu, kundi la Ansar al-Sharia na al-Qaida ni pande mbili za sarafu moja. Ansar al-Sharia inaibua tishio linaloendelea, ikiwa ni dawa [mahubiri] mwendelezo wa al-Qaida. Ninamaanisha inaweza kuwa sehemu ya kile tunachoweza kukizingatia kuwa ni uanzishaji upya wa uhusiano kati ya wanajihadi wa Kisalafi na jamii za Kiislamu.
Tabia ya al-Qaida ni kutegemea kabisa vurugu na vitendo vya kutumia silaha zilizowafikisha katika kudorora na kuzidi kuanguka.
Ansar al-Sharia, kwa sasa, imekuja kupata uhakika wa pingamizi na ujitengaji huu ambao al-Qaida inakumbana nao. Huu ni umuhimu wa wito wa bin Laden ambaye aliagiza wafuasi wake kufikiria kuhusu jina jipya kwa ajili ya asasi ambayo itaweza kurejea kwa jamii katika sura mpya ambayo itaweza kukubalika, lakini bila kuachana na itikadi ya wanajihadi wa Kisalafi, yaani bila ya mageuzi ya itikadi yoyote.
Sabahi: Ni zipi sababu za kuanguka kuungwa mkono kwa al-Qaida?
Rami: Sababu ya msingi zaidi ni kwamba vyombo vya habari vimeacha kutangaza kuhusu al-Qaida, na halafu kumekuwa na majeshi yaliyobanwa na kuzingirwa kwa usalama katika mifumo na alama za al-Qaida. Mwanzoni, al-Qaida ilitegemea sana vituo vya satelaiti kutangazia oparesheni zao kama njia kuu ya kutangaza jina lake, kutuma ujumbe wake na kuitangaza asasi hiyo katika nchi za Kiislamu, na kupitia hilo, ilipanua mzunguko wa wapenzi wao na wanaotoa misaada katika nchi hizi. Hii ni nyongeza ya kimsingi katika wajibu wa maandiko ya al-Qaida katika intaneti.
Hata hivyo, vipigo ambavyo al-Qaida imepata, jeshi lililobanwa, usalama na vyombo vya habari vinavyoizingira, na kuachia operesheni zao zilizofanya usimamizi mkuu kuzidi kupungua hadi kufikia mwaka 2005, na matokeo yake, mzunguko wa wapenzi wao na wanaowasaidia yamekuwa hai zaidi kuliko al-Qaida yenyewe.
Kwa kuzingatia hilo, walifikiria kuhusu mahitaji ya kuanzisha kanuni mpya ya kufanya bahati nasibu kuhusu dawa kama njia ya kupanuka, kujipenyeza, na kupatanisha mizizi yake katika jamii kupitia matumizi ya mimbari, fursa za kijamii na kazi za kujitolea ambazo zipo karibu na watu. Chemu chemu ya Uarabuni imechangia katika awamu hii kwa kuleta kiwango kikubwa cha uhuru kwa vikundi vya Wasalafi pamoja na kiwango kinachokua cha uhuru baada ya jamii za kidini kujisafisha zenyewe kwa usalama imara, kwa mara ya kwanza baada ya udikteta wa zamani.
Sabahi: Nini asili ya ushirikiano baina ya al-Qaida na Ansar al-Sharia? Je, kuna uhusiano wowote wa uongozi na viongozi wakuu?
Rami: Kiungo kikubwa kati ya pande hizo mbili ni ulinganifu wa kiitikadi. Ansar al-Sharia wako ndani ya makundi ya kiitikadi yanayoendana na al-Qaida, na wote wanatangaza utii kwa kamanda wa al-Qaida huko Waziristan, ingawa hakuna uhusiano wa kiasasi.
Hili ni wazi, kama vile tukio lililotokea huko Yemen, ambapo al-Qaida walikuwapo pamoja na Ansar al-Sharia. Kimsingi wanafanana na wako karibu sana, lakini hawafanyi kazi katika wigo mmoja. Kwa kuhitimisha, inaweza kuelezwa kwamba Ansar al-Sharia wanawakilisha mkono itikadi ulio na mfumo fulani katika wigo mpana wa wanajihadi wa Wasalafi, wakati al-Qaida wanawakilisha mkono wa jeshi lake linalotumia silaha. Kwa maneno mengine, Ansar al-Sharia ni sura ya kiitikadi, wanaotoa misaada ya kibinadamu na fedha kwa jeshi la al-Qaida.
Mantiki ya Kisalafi yakataa demomkrasia
Sabahi: Ni yepi matarajio ya kisiasa ya Ansar al-Sharia?
Rami: Mfumo wa kisiasa ambao vikundi hivi vinaahidi ni kuanzisha mfumo wa kikhalifa mfano wa Talibani kupitia jihadi. Mantiki ya kisalafi inakataa aina zote za siasa za wananchi na utawala wa kiraia. Ansar al-Sharia haiwezi kukataa demokrasia, kwa sababu demokrasia inaweza kumuweka mwanamke katika utawala, na pia inaweza kumuweka mtu mwenye msimamo wa kati au Mkristo; kitu ambacho Wasalafi hawawezi kukikubali daima. Hawawezi kukubali chochote kisichokuwa utawala wa sharia, na utawala wa sharia kwa dhana yao ni ule ulioidhinishwa na mfumo wa Kitalibani.
Hili linaweza kuonekana katika maeneo ambayo Wasalafi wanayadhibiti huko Mali, Somalia na Yemen kwa sababu ya udhaifu wa serikali kuu na uhatarishi wa tawala za kisiasa. Katika maeneo hayo, wao ni sawa sawa na mfumo wa Kitalibani wa serikali na uongozi, utaratibu huo huo na hakuna jipya zaidi.
Kitu muhimu kwao ni kuanzisha jeshi la polisi lenye maadili kwa ajili ya kuimarisha nguvu na kuzuwia maovu, baadaye kuchoma moto maduka video kaseti na maduka ya vileo, kuwatenganisha wanawake na wanaume, kuzuwia programu za elimu, kuharibu maeneo ya makaburi ya kidini na kuondosha aina yoyote ya vitu wanavyovichukulia kuwa vinakwenda kinyume na sharia.
Hii maana yake ni kuwa tunakabiliwa na mambo yale yale ya utawala wa Taliban.
No comments:
Post a Comment