Tuesday, October 2, 2012

KIIZA BESIGYE MIKONONI MWA POLISI TENA UGANDA.

Posted: 1st October 2012 by MillardAyo in News
.
Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Uganda cha Forum for democratic change –FDC-kanali Kiiza Besigye amekamatwa na polisi mjini Kampala kwa kile polisi wanasema ni kushawishi wananchi kujiunga katika maandamano haramu.
Dr Kiiza Besigye amekamatwa na askari polisi wa kuzuia fujo baada ya purukushani kati ya polisi na baadhi ya wafuasi wake ambapo polisi walikua wanamvuta kumuingiza katika karandinga ya polisi huku wafuasi wake wakimvuta kwa nje lakini polisi ndio walifanikiwa baadae.

BBC wameandika Naibu msemaji wa polisi Vicent Ssekatte kawaambia wandishi wa habari kwamba Besigye amekamatwa kutokana na kuchochea wananchi kufanya fujo.
Hatua hii imekuja baada ya Besigye na viongozi wengine wa upande wa upinzani chini ya vuguvugu la 4GC (For God and My country) kutangaza mwishoni mwa juma kuanzisha walichoita mchakato wa matembezi ya uhuru- Walk to freedom kupinga walichoita ufisadi, utawala mbaya na mengine. Ilikuwa imepangwa kuanza Jumatatu.

No comments:

Post a Comment