Friday, October 19, 2012

RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN AZUNGUMZA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA CHWAKA MKOA WA KUSINI UNGUJA


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chwaka kuhusu mzozo wa uvuvi kwa wananchi hao na ndugu zao wa kijiji cha Marumbi, katika uwanja wa Skuli ya kijijini hapo jana, pia aliwaomba kuwa kitu kimoja kuondosha tofauti zao.
 Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Chwaka wakimsikiliza rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na wananchi hao alipofanya ziara maalum, kuhusu mzozo wao wa uvuvi na wananchi wa kijiji cha Marumbi Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akiwapungia mkono wananchi wa kijiji cha Chwaka kama ishara ya kuwaaga, baada ya mazungumzo, hayo.
(Picha na Ramadhan Othman, Ikulu)

No comments:

Post a Comment