
Mchungaji Kiongozi Michael Meela wa Kanisa la Efatha mkoani Rukwa akiongelea kuhusu suala hilo alisema hasara iliyopatikana ni zaidi ya shilingi milioni 228 na kwamba tukio hilo lilitokea mara tu baada ya Mbunge wa Jimbo la Kwela Mh. Ignas Malocha kuhutubia mkutano wa hadahara kijijini hapo na kuwahamasisha wananchi watumie nguvu ya umma kuyakomboa mashamba yao yaliyochukuliwa na mwekezaji huyo.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Rukwa Bw Jacob Mwaruanda akithibitisha kuhusu sakata hilo alisema tayari wanawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kufanya uharibifu huo mkubwa namsako unaendelea kuwatafuta wengine waliohusika katika tukio hilo.
Chanzo mjengwa blog
No comments:
Post a Comment