Monday, October 1, 2012

VODACOM YACHANGIA UANZISHWAJI MFUKO WA WALEMAVU ZANZIBAR


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akifurahia jambo na Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Bw Salum Mwalim mara baada ya kupokea hundi yenye thamani ya shilingi Milioni Kumi na Tano mchango wa Vodacom Foundation kwenye mfuko wa maendeleo ya watu wenye ulemavu Zanzibar. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Idara ya Mahusiano na Mawasiliano wa Vodacom Bi Joseline Kamuhanda. Vodacom ilikabidhi hundi hiyo katika hafla ya uzinduzi wa mfuko huo iliyofanyika mwishoni mwa wiki Mjini Zanzibar.Mkuu wa Idara ya Mahusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Bi Joseline Kamuhanda.akitoa salaam za Vodacom Tanzania wakati wa hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar kuchangia mfuko mpya wa maendeleo ya watu wenye ulemavu Zanzibar iliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini Zanzibar. Vodacom Tanzania ilichangia Shilingi Milioni Kumi na Tano kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii - Vodacom Foundation.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kutoka kushoto Meneja Mahusiano ya Nje Bw. Salum Mwalim, Mkuu wa Idara ya Mahusiano na Mawasiliano Bi. Joseline Kamuhanda na Meneja Kanda ya Zanzibar Bw. Mohamed Mansour wakipokea utambulisho wa kuwa miongoni mwa wadhamini wakuu waanzilishi wa mfuko wa Manedeleo ya watu wenye ulemavu Zanzibar wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfuko huo iliyofanyika mwishoni mwa wiki Zanzibar. Wa kwanza kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Zanzibar Mh. Said Ali Mbarouk.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akihutubia wadau mbalimbali waliohudhuria hafla ya chakula cha jioni  iliyolenga kuuzindua rasmi mfuko wa maendeleo ya watu wenye ulemavu Zanzibar mwishoni mwa wiki mjini Zanzibar. Wa kwanza kushoto ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad. Hafla hiyo iliandaliwa na Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Vodacom Tanzania ilichangia Shilingi Milioni Kumi na Tano kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii - Vodacom Foundation.
 ------
Taarifa kwa vyombo vya habari.
VODACOM YACHANGIA UANZISHWAJI MFUKO WA WALEMAVU ZANZIBAR
·        Yachangia 15M. Ni mfuko mpya maalum wa serikali
·        Yalilia juhudi zaidi kukomboa walemavu
·        Vodacom Foundation kuendeleza misaada zaidi Zanzibar
Septemba 30, 2012… Ikikadiriwa kuwa na watu wenye ulemavu wapatao 9000 Visiwani Zanzibar, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanzisha mfuko maalum wa maendeleo ya watu wenye ulemavu hatua iliyoungwa mkono kwa dhati na kampuni ya Vodacom Tanzania kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii”Vodacom Foundation”kwa kuchangia Shilingi 15 Milioni.
Vodacom Foundation imechangia fedha hizo katika hafla maalum ya kuchangisha fedha iliyoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya umma na binafsi katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort,Mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki.
“Vodacom Tanzania inaipongeza sana serikali ya Zanzibar hasa Ofisi ya Makamu wa Rais wa Kwanza kwa kuchukua hatua za ziada kubuni njia za kusaidia jamii ya watu wenye ulemavu ambao wanakabiliwa na changamoto kadhaa za kimaisha, Hili ni jambo jema na tunlaiunga mkono” Alisema Mkuu wa Mawasiliano na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Bi. Joseline Kamuhanda Bi Kamuhanda akimueleza Rais wa Zanzibar Dk. Shein.
Kabla ya kukabidhi hundi ya mfano wa fedha hizo Kamuhanda alisema Vodacom Tanzania inatoa fedha hizo kupitia mfuko wake wa Vodacom Foundation wenye shabaha ya kusaidia juhudi za ustawi wa jamii nchini kwa kutambua umuhimu wa mchango wa sekta binafsi kuunga juhudi za serikali za kuboresha maisha ya watu.
“Tunapongeza juhudi zako Mheshimiwa Rais Dk. Shein na kipekee tunampongeza Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad kwa ubunifu wa kuanzisha mfuko huu, ni imani yetu kwamba shabaha ya uanzishwaji wake itafikiwa na kuleta faraja kubwa kwa ndugu zetu wenye ulemavu.” Aliongeza Joseline Kampuni ya Vodacom kupitia Vodacom Foundation imekuwa ikichangia juhudi mbalimbali za kijamii Zanzibar katika maeneo ya elimu, afya, uwezeshaji wananchi kiuchumi hususan wanawake kupitia mradi wa MWEI na imeahidi kuendelea kufanya hivyo.
“Shabaha ya kampuni ya Vodacom hapa nchini sio tu biashara bali pia kuona maisha ya jamii  zinazotuzunguka yananufaika na uwepo wetu kazi inayofanywa kupitia Vodacom Foundation na ndio maana leo Mh. Rais Vodacom ni moja ya wahisani wakuu waliofanikisha kuanza kazi kwa mfuko huu.” Aliongeza Joseline
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  Dk. Mohammed Shein akizungumza katika hafla hiyo aliwashukuru wadhamini waliowezesha kupatikana kwa fedha za kuanza kwa mfuko huo Vodacom Tanzania ikiwa moja ya wadhamani wakuu na hivyo kuzinduliwa rasmi na kutoa rai kwa michango ili kasi iliyoanza nayo mfuko huo iwe endelevu huku Makamu wa kwanza wa Rais, Maalim Seif, akiuelezea mfuko huo kuwa umelenga kuwezesha watu wenye ulemavu kujiajiri, mafunzo, uwezeshaji, afya, unyanyapaa n.k
Mfuko huo upo chini ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na kuanzia sasa watu mbalimbali wanauwezo wa kuchangia kutumia huduma ya Vodacom M – pesa kupitia namba 0755 222666,namba maalum iliyo tolewa kwa hisani ya Vodacom ili kurahisisha uchangiaji wa fedha katika mfuko huo.

No comments:

Post a Comment