Wednesday, December 12, 2012

WASHINDI WA VODACOM APPSTAR CHALLENGE WATEMBELEA OFISI ZA VODACOM


KARIBUNI: Washindi wa ndani wa  Mashindano ya Teknolojia ya  AppStar  Roman Mbwasi (katikati) na Ernest Mwalusanya wakiwa pamoja na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na masoko wa Vodacom, Kelvin Twissa (kulia), walipomtembelea Ofisini kwake kabla ya kuondoka kwenda nchini Afrika ya Kusini kwa ajili ya mashindano ya kimataifa ya Vodacom AppStar.
KWAHERINI: Washindi wa ndani wa  Mashindano ya Teknolojia ya  AppStar Roman Mbwasi (wa pili kushoto) na Ernest Mwalusanya wakiwa pamoja na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na masoko wa Vodacom, Kelvin Twissa (kulia), walipomtembelea ofisini kwake kumuaga kabla ya kuondoka kwenda Afrika ya Kusindi katika Mashindano ya kimataifa ya AppStar. Pamoja nao ni kiongozi wa safari hiyo Meneja wa Miradi na Mawasiliano wa Vodacom, Erica Luis (kushoto).
TUTAWAKILISHA VIZURI: Washindi wa ndani wa  Mashindano ya Teknolojia ya  AppStar  Roman Mbwasi (katikati) na Ernest Mwalusanya wakiwa pamoja na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na masoko wa Vodacom, Kelvin Twissa (kulia), wakifurahia jambo wakati washindi hao walipotembelea Ofisi za Vodacom kabla ya kuondoka kwenda kwenye Mashindano ya kimataifa ya AppStar.
---
Washindi wa Vodacom AppStar Challenge leo watembelea Ofisi za Vodacom kabla ya kukwea pipa kwenda Afrika ya Kusini, kuiwakilisa Tanzania katika Mashindano ya kimataifa ya Teknohama ya Vodacom AppStar. Mashindano hayo yametoa nafasi kwa vijana wa Kiafrika kuonyesha vipaji vyao katika Nyanja ya Teknolojia kwa kutengeneza program za kompyuta na simu. Nchi zinazoshiriki katika mashindano hayo ni Misri, Lesotho, Tanzania, Afrika ya Kusini na Qatar

No comments:

Post a Comment