Na Mwandishi Wetu
Shule ya Msingi ya Kibamba katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam inakabiliwa na uhaaba wa madawati 500, jambo linalowalazimu wanafunzi wa shule hiyo kukaa chini wakati wakifundishwa darasani.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Asia Mpate alibahanisha hayo jana na kusema kuwa shule yake yenye wanafunzi 1,950,kuliwa na madawat 320 na madarasa 13 tu.
Mwalimu Mkuu huyo alikuwa akizungumza kwenye hafla ya kukabidhiwa misaada na Benki ya KCB iliyotoa madawati 25, meza tatu, viti vya walimu sita, madafyari 235 na peni 200 , vyote vikiwa na thamani ya Sh, Milioni 5 kwa shule hiyo.
Alisema kuwa uhaba mkubwa wa madawati katika shule yake kumepelekea utoro mkubwa kwa wanafunzi wake kwani wanafunzi wake hulalamikia hali mbaya na ugumu wa kukaa chini sakafuni.
Mpate amesema kuwa wanafunzi wengi wa shule yake wamechanganyikiwa na hali hiyo na hivyo huamua kutohudhuria masomo, jambo linaofanya ufanisi mdogo wa elimu kwa wanafunzi wake.
" Utoro ni mkubwa katika shule yetu kwa sababu hali halisi ya madarasa ni ya kutisha, hatuna madarasa ya kutosha wala vitendea kazi . Tunashukuru Benki ya KCB kwa msaada wao ambao tunaamnini kuwa utatusaidia kuboresha kiwango cha elimu katika shule yetu", alisema mwalimu mkuu huyo..
Kwa upende wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo, Dk Edmund Mndolwa alisema kuwa msaada huo ni sehemu ya wajibu wake wa benki kusaidia jamii na kwamba benki yake imejidhatiti kusaidia kuinua kiwango cha elimu nchini Tanzania.
Aliwashauri wanapokea misaada ya benki hiyo kutumia ipasavyo na inavyotakiwa misaada inayotolewa na benki yake.
Kwenye hafla hiyo pia benki ya KCB ilitoa msaada wa madawati 64 yenye thamani ya Sh. Milioni tano kwa Shule ya Msingi ya Makumbusho pia ya jijini .
Wakati huo huo hopsitali ya Sinza ya jijini Dar es Salaam imepokea msaada wa vifaa vya hospitali vyenye thamani ys Sh. Milioni 7.4 kutoka kwa Benki ya KCB katika hafla iliyofanyika kwenye hopsitali hiyo jana.
Dokta Mwandamizi wa hospitali hiyo, Dk Benedict Luwoga alishukuru benki hiyo kwa msaada huo na kusema kuwa vifaa hivyo vilikuja kwa wakati na kuvitaja vifaa hivyo ni pamoja na vitanda vinne vya kuzalisha kwa mama wajawazito.
Alisema kuwa hospitali yake ilizidiwa uwezo kwa sababu ilikuwa na vitanda viwili tu vya kuzalisha mama wajawazito , kwa hiyo vitanda hivyo vinne zaidi ilikuwa ni ukombozi mkubwa kwa hospitali yake.
"Tunashukurui Benki ya KCB kwa msaada huo, umekuja kwa wakati ambapo hospitali ilikuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi. Amezitaka kampuni zingine ziige mfano wa benki ya KCB", alisema Dk Luwoga.

No comments:
Post a Comment