Tuesday, January 29, 2013

NIGERIA, BURKINA FASO NAO WATINGA ROBO FAINALI AFCON 2013


Mikel John Obi  wa Nigeria (katikati) akiwatoka wachezaji wa Ethiopia, Dawit Estifanos na Getaneh Kebede wakati wa mechi yao ya Kombe la Mataifa ya Afrika iliyochezwa leo katika Uwanja wa Royal Bafokeng, Rustenburg nchini Afrika Kusini. Nigeria wameshinda bao 2-0 na kufanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali. Mabao ya Nigeria yote yamefungwa na Victor Moses.
Collins Mbesuma wa Zambia akituliza mpira kifuani pembeni ya Djakaridja Kone wa Burkina Faso wakati wa mchezo wao wa Kombe la Mataifa ya Afrika uliopigwa leo katika Uwanja wa Mbombela nchini Afrika Kusini. Timu hizo zimetoka sare ya 0-0 na Burkina Faso kufanikiwa kutinga Robo Fainali ya michuano hiyo.
(PICHA NA MTN FOOTBALL)

No comments:

Post a Comment