Mmoja wa Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Andrew Chenge akiwasilisha maoni ya chama chake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo Januari 7, 2013 katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba (kulia) wakiongozwa na Dkt. Salim Ahmed Salim wapokea maoni kuhusu Katiba Mpya kutoka kwa uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ulioongozwa na Mwenyekiti wake Ndg. Freeman Mbowe katika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam leo Januari 7, 2013
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba akiwasilisha maoni ya chama chake kuhusu Katiba Mpya mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Jumatatu, Jan 7, 2013) katika Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba na kulia kwa Prof. Lipumba ni Katibu wa Tume Assaa Rashid.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba katika picha ya pamoja na Viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) wakiongozwa na Mwenyekiti wao Prof. Ibrahim Lipumba mara baada ya chama hicho kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya kwa Tume jijini Dar es Salaam leo Januari 7, 2013.
(Picha kwa hisani ya WWW.HAKINGOWI.COM)
No comments:
Post a Comment