MOHAMED MATUMLA AMGALAGAZA NASSIBU RAMADHANI KWA POINTI,AIBUKA NA PIKIPIKI
Bondia Mohammed Matumla (kushoto) akimwadhibu Nassibu Ramadhani wakati wa mpambano wao wa raundi kumi uliofanyika siku ya sikukuu ya Krismasi na kugombania pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni 1.9 Matumla alishinda kwa pointi mpambano huo na kuibuka na bodaboda. Bondia Mohamed Matumla (kushoto) akipambana na Nassibu Ramadhani wakati wa mpambano wao uliofanyika jana ambapo Matumla alishinda kwa pointi. Bondia Lulu Kayage (kushoto) akipambana na Mariam Abdallah wakati wa mpambano wao wa kusherehekea sikukuu ya Krismasi. Kayage alishinda kwa K.O. Bondia Hamis Ajari (kushoto) akipambana na Cosmas Cheka wakati wa mpambano wao uliofanyika wakati wa sikukuu ya Krismasi jana. Cheka alishinda kwa pointi. Bondia Sadiq Abdulazizi (kushoto) akipambana na Juma Fundi wakati wa mpambano wao uliofanyika wakati wa sikukuu ya Krismasi. Juma Fundi alishinda kwa pointi. Baadhi ya mashabiki wakifuatilia mpambano huo uliokuwa mkali na kutoa burudani ya aina yake kwa mashabiki nchini.
No comments:
Post a Comment