Monday, March 3, 2014

The Advantages of Eating Beans Faida Za Kula Maharage!

Maharage ni chakula cha bei nafuu na ni chakula chenye protini  nyingi yenye faida. Tumia maharage kwenye kachumbari, supu, mchuzi, kande, mboga ya ziada au yafanye kama mafuta mbadala katika vyakula vya kuoka. Maharage yana virutubisho vingi and vinaweza kusiaidia kuzuia magonjwa ya moyo, kisukari na saratani. Idara ya Kilimo ya Marekani inashauri wanawake kula kikombe kimoja na nusu cha maharage kwa wiki na wanaume kula vikombe viwili vya maharage.
 Virutubisho
Ingawa aina halisi ya virutubisho itokanavyo na maharage inalingana na aina ya maharage unayokula, lakini maharage ina calories (calories /nguvu) takribani 116 katika nusu kikombe, ina pia gramu nane (8) za protini, sita (6) za fauba na ni kama haina mafuta kabisa. Maharage ni chanzo kizuri sana cha fiber, kopa, folate, chuma, magnesium, manganese, phosphorus, potassium na zinc. Kwa kua fiber na protini nyingi inakufanya ujisike umeshiba hivyo kula calories chache na hivyo kukusaidia kuweza kuwa na uzito mzuri.
Moyo Wenye Afya
Maharge yanatabia kadhaa ambazo zinafanya moyo kuwa wenye Afya Njema, hii ni kutokana na makala iliyochapishwa na “British Journal of Nutrition”. Maharage yanamafuta kidogo, na yana fiber inayoyeyuka na ina kemikali (phytochemiclas), vyote ambavyo vinasaidia kupunguza wingi wa cholesterols. Folate ipatikanayo katika maharage pia ina faida kwakuwa inasaidia kupunguza wingi wa homocysteine, tindikali (amino acid) ambayo inaongeza hatari ya kupata magonjwa ya moyo ikipatikana kwa wingi kwenye damu.
Kisukari
Kula maharage kwa wingi inaweza kupunguza aina ya Kisukari kiitwacho Type 2-Diabete, hii ni kutokana na utafiti uliochapishwa Januari 2008 katika Jarida la “American Journal of Clinical Nutrition”. Watu waliokula maharage zaidi walikuwa na uwezekano mdogo zaidi ya kupata kisukari katika kipindi cha utafiti huu, labad ni kutokana na fiber na antioxidants inayopatikana katika maharage au kutokana na glycemic indes katika maharage ukilinganisha na vyakula vingine vyenye wanga. Glycemic index inapima madhara ya vyakula vyenye wanga katika sukari ya damu na vyakula vyenye index ndogo huwa na sukari ndogo katika damu.
 Saratani
Utafiti uliochapishwa na “Cancer Epidemiology, Biomarkers & Prevention”

No comments:

Post a Comment