Monday, June 16, 2014

WIKI YA UTUMISHI WA UMMA YAFANYIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA DAR


Wasanii wa JKT Mgulani wakijiandaa kuburudisha kwa ngoma ya Msewe.
Kapteni Makungu (kushoto), Daud Kayanda na Dorin Chacha wakiwa katika banda la Jeshi la Kujenga Taifa katika maadhimisho ya Utumishi wa Umma.
Kijana akipata maelezo kutoka kwa mfanyakazi wa Mfuko wa Pensheni kwa Wafanyakazi (PPF).
Hii ni mashine maalumu kwa ajili ya kuchanganyia vyakula vya mifugo toka Suma JKT.
Mgeni Rasmi ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, George Mkuchika, akipata maelezo kutoka kwa ofisa wa banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Suma JKT wakiwa na zana za kilimo.
Bendi ya Serengeti ikitumbuiza katika maadhimisho hayo.
Umati wa watu uliofika Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Mwananchi akijitolea damu katika hafla hiyo.
Mgeni Rasmi George Mkuchika, akisoma risala ya ufunguzi.
Mlemavu akisikilizwa na mhudumu wa banda la Bima ya Afya.
Moja ya mabango kuhusu hafla hiyo yaliyokuwa uwanjani.
MAADHIMISHO ya Wiki ya Utumishi wa Umma yamefunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, George Mkuchika, leo 16 Juni mwaka huu ambapo yataendelea hadi Juni 23  katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ambapo yalisindikizwa  kwa michezo na burudani mbalimbali.
(Picha na Gabriel Ng’osha/GPL)

No comments:

Post a Comment