Monday, July 14, 2014

JHIKOMAN ATEMBELEA SHULE YA MUZIKI YA REUTLINGEN, UJERUMANI

Darasa la muziki katika taasisi ya Shule ya Muziki Reutlingen ,Ujerumani.Jhikoman akiwafundisha wanafunzi kutumia gitaa katika Shule ya Muziki Reutlingen.Jhikoman akiwa kama mwalimu mwalikwa katika shule hilo.Mwanamuziki Jhikoman akiendelea kuwapa somo wanafunzi.
Tubingen, Ujerumani
MWANAMUZIKI maarufu wa Reggae barani Afrika, Jhikoman ambaye yupo katika ziara ya kikazi barani ulaya, juzi alitua katika mji wa Tubingen, Ujerumani kwa ajili ya kushiriki katika maonyeso makubwa ya Kimataifa ya African Festival Tubingen 2014 ambako amealikwa na shirika la Afrikaktiv Org.
Jhikoman amelamba dili la mkataba wa kudumu wa kutumbuiza katika onyesho hilo, pia amepata nafasi za kualikwa na kutembelea miradi mbalimbali ya utamaduni nchini Ujerumani zikiwemo shule na taasisi za muziki, ambazo amekuwa kivutio kikubwa na taasisi hizo zimeahidi kwenda Bagamoyo kwa kupata ujuzi zaidi wa kimuziki na utamaduni.

No comments:

Post a Comment