STAA wa vichekesho nchini Marekani, Tracy Morgan, ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kukaa wiki tano tangu alipopata ajali iliyomuua mwenzake Jimmy Mack.
Morgan alivunjika mguu na mbavu baada ya gari alilokuwa akiendesha kugongwa kwa nyuma huko New Jersey, Marekani Juni 7 mwaka huu.
Katika ajali hiyo, mchekeshaji James McNair, maarufu kwa jina la Jimmy Mack alifariki dunia huku mchekeshaji Ardley Fuqua na abiria mwingine aitwaye Jeffrey Millea, wakijeruhiwa.
No comments:
Post a Comment