Sunday, August 19, 2012

BENKI YA KCB TANZANIA YAKABIDHI MSAADA WA VYAKULA KWA VITUO 6 VYA KULELEA WATOTO YATIMA SIKUKUU YA ID


Mkurugenzi wa benki ya KCB Tanzania, Bw. Nikubuka Shimwela (kulia) akiwakabidhi msaada wa vyakula mbalimbali kwa ajili ya sikukuu ya Idd watoto waishio katika mazingira magumu wa kituo cha Yatima Group Trust Fund cha Mbagala jijini Dar es Salaam. kushoto ni Mjumbe wa bodi wa benki hiyo Bi. Zuhura Muro.
Mkurugenzi wa benki ya KCB Tanzania, Bw.Nikubuka Shimwela, (kulia) akimkabidhi Mkuu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Madina Children Home kilichopo Tandale jijini Dar es Salaam, msaada wa ndoo ya mafuta ya kupikia ikiwa ni sehemu ya vyakula mbalimbali vilivyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya sikukuu ya Idd, katikati ni Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Bi.Christina Manyenye.
Mjumbe wa Bodi wa benki ya KCB Tanzania Bi.Zuhura Maro akiwakabidhi msaada wa mbuzi watoto wa kituo cha yatima cha  Al-Madina Children Home kilichopo Tandale jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya sikukuu ya Idd, kushoto ni Mkurugenzi wa benki hiyo Bw.Nikubuka Shimwela,Mlezi wa kituo hicho Bi.Kuruthumu Yusuph na Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Bi.Christina Manyenye.
Mkurugenzi wa Benki ya KCB Tanzania Bw.Nikubuka Shimwela,akimakabidhi Mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Malaika kilichopo Mwananyamala jijini Dar es Salaam, Najma Manji,msada wa mbuzi kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Idd kwa watoto wa kituo hicho jumla ya vituo sita vya kulelea watoto yatima vilikabidhi misaada hiyo,Katikati ni Mjumbe wa Bodi wa benki Bi.Zuhura Maro.
Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB Tanzania Bi.Christina Manyenye akimkabidhi Mlezi wa kituo cha kulea watoto yatima cha Hissani cha Mbagara jijini Dar es Salaam,Idaya Shukrani msaada wa boksi ya sabuni ulioambatana na vyakula mbalimbali kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Idd,
Meneja wa benki ya KCB Tanzania tawi la Kariakoo jijini Dar es Salaam, Bw.Clement Mwanzalima,akimkabidhi Mlezi wa kituo cha kulea watoto yatima cha Hissani cha Mbagala jijini Dar es Salaam,Idaya Shukrani msaada wa boksi ya sabuni ulioambatana na vyakula mbalimbali kwa ajili ya watoto wa kituo hicho kusherehekea sikukuu ya Idd.

No comments:

Post a Comment