
Mlinzi wa kati wa timu ya APR kutoka nchini Rwanda Mbuyu Twite
amekamilisha usajili wake ikiwa ni pamoja na kupata uhamisho wa
kimataifa ITC na kuweza kujiunga na mabingwa wa kombe la klabu Bingwa
Afrika Mashariki na Kati kombe la Kagame timu ya Young Africans Sports
Club.
Mbuyu Twite ambaye zoezi lake la usajili lilianza takribani wiki
mbili zilizopita limefikia mwisho baada ya klabu ya Young Africans
kufanikiwa kupata uhamisho wake wa kimataifa kutoka timu aliyokuwa
akiichezea ya APR ambapo awali alikuwa akiichezea timu ya Lumpopo st.
Twite ambaye alingara sana katika mashindano ya Kagame yaliyomalizika
hivi karibuni na Young Africans kuibuka mabingwa, amesema anajisikia
furaha na mwenye bahati kufanikiwa kujiunga na mabingwa mara mbili
mfululizo wa kombe la Kagame.
Usajili wa Twite ulianza takribani wiki mbili zilizopita ambapo
mjumbe wa kamati ya Utendaji wa klabu ya Young Africans Abdallah Bin
Kleb aliamua kwenda nchini Rwanda kuhakiksiha zoezi hilo linakamilika
haraka ipasavyo, ambapo mara baada ya kumalizana na Twite aliendelea
kuhakikisha anafuatilia ITC yake.
Akiongea na www.youngafricans.co.tz Bin
Kleb amesema, Young Africans ni timu kubwa katika Ukanda huu, Viongozi
wake wanafanya mambo yao kwa uhakika zaidi, hivyo hawakutaka kuongelea
suala la Twite mpaka watakapoona wamekamilisha zoezi lote'
"Unajua usajili sio mchezaji kusajuli makaratasi ya mkataba tu, kuna
kupata barua ya kumruhusu kutoka timu anayotoka, uhamisho wa mchezaji
kutoka chama husika cha soka cha nchi, baada ya hapo ndio unaweza
kutangaza sasa kwamba ni mchezaji wako halali"alisema Bin Kleb.
Kusajiliwa kwa Mbuyu Twite kunaifanya timu ya Young Africans kuwa na
ukuta wa walinzi wa kimataifa akiwemo Kelvin Yondani, Nadir Haroub
Cannavaro, Ladislau Mbogo na Ibrahim Job kwa nafasi ya ulinzi wa
katikati.
Twite anatarajiwa kuwasili mapema wikii kuungana na wacheji wenzake
katika mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara
inayotarajiwa kuaanza sepetemba mosi.
No comments:
Post a Comment