
Chris Lukosi akiwa na Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Kenya tawi la Sudan Kusini, Mariha Nyaliet Chol.
Chris Lukosi akiwa katika pozi.
KAMPUNI ya usafirishaji wa mizigo ya Serengeti Freight Forwarders Ltd yenye makao yake jijini London, Uingereza, inategemea kufungua ofisi zake nchini Kenya na Sudan Kusini hivi karibuni.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Chris Lukosi, jana alipokuwa akihudhuria mkutano wa raia wa Kenya walioko nchi za nje (Kenyan Diaspora) uliofanyika jijini London, Uingereza, ambako alialikwa kama mmoja wa wajasiriamali wakubwa kutoka Afrika Mashariki.
Katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Ubalozi wa Kenya nchini Uingereza, Lukosi alikutana na Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Kenya, Samuel Phoghisio, Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Kenya tawi la Sudan Kusini, Mariha Nyaliet Chol, na Mkuu wa Huduma wa Kenya Commercial Bank (KCB) tawi la Tanzania, Shose Kombe.
Serengeti Freight Forwarders Ltd ni kampuni inayokua kwa kasi nchini Uingereza
No comments:
Post a Comment