Monday, August 27, 2012

Simba kumtunukia heshima Ulimboka

Ulimboka Mwakingwe.
Na Khadija Mngwai

UONGOZI wa Simba umesema unaandaa sherehe maalum ya kumuaga aliyekuwa mchezaji wake, Ulimboka Mwakingwe, baada ya kuichezea timu hiyo kwa muda wa miaka 10 hadi kufikia hatua ya kustaafu soka.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema klabu hiyo itaandaa mechi maalum ambayo Ulimboka atacheza huku akiwa amevaa jezi yake namba 14, ikiwa ni ishara ya kumuenzi pamoja na kumtunukia heshima maalum ya kuichezea timu hiyo kwa muda wote huo.

“Mchezaji wetu Ulimboka Mwakingwe amestaafu soka rasmi, hivyo uongozi utaandaa sherehe maalum ya kumuaga, ikiwa ni pamoja na kumtunukia heshima maalum kutokana na kuichezea Simba kwa muda mrefu.

“Katika sherehe hizo,…

“Katika sherehe hizo, mchezaji huyo atacheza mechi moja ya kuagwa na timu tutakayoitafuta hapo baadaye na atavaa jezi yake namba 14 ikiwa ni ishara ya kumpa heshima,” alisema Kamwaga.
Alisema kuwa kufanya hivyo kutamsaidia mchezaji huyo kufarijika kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa kwa Simba katika muda wote alioitumikia klabu hiyo.
Ulimboka alishindwa kumalizia ligi msimu uliopita kutokana na kukabiliwa na kesi ya kutoa rushwa kwa kipa wa Mtibwa Sugar, Shaban Kado, ili aachie mabao katika mechi ya Simba dhidi ya timu hiyo msimu wa 2010/11. Wakati huo yeye alikuwa Majimaji.

No comments:

Post a Comment