Adebayor aliuambia mtandao wa Tottenham:
"Namba 10 ni namba maalum kwanguna hivyo ilivyokuwa haina mtu nikaomba kama naweza kubadilishiwa namba ya jezi na klabu ikawa haina pingamizi juu ya hilo.
"Lakini walikuwa na wasiwasi juu ya jezi ambayo walishaiweka sokoni na mashabiki wakawa tayari wameshanunua ikiwa imeshandikwa jina la namba 25 tayari kwa msimu mpya.
"Ninajisikia furaha sana kwa kuwa mashabiki wa Spurs wanataka kuvaa jezi yenye namba na jina langu na sikutaka waathiriwe na mabadiliko niliyoyataka. Hivyo, nina furaha kubeba gharama za kuwawezesha mashabiki wote walionunua jezi mara kwanza kubadilisha kutoka Adebayor 25 - kwenda Adebayor 10.
No comments:
Post a Comment