Friday, September 21, 2012

AFRIKA NGOMA BAND YAWAPAGAWISHA MASHABIKI UJERUMANI


Ngoma Africa Band aka FFU wakiwa kazini.
Mashabiki wakipagawishwa na burudani iliyokuwa ikishushwa na FFU.
Jumba la ajabu la "Klimahaus  Arena” mjini Bremerhaven, walipofanyia shoo FFU.
Kikosi kazi cha  FFU.
KIKUNDI  cha wanamuziki wa Tanzania kijulikanacho kama  Ngoma Africa Band aka FFU chenye  maskani yake nchini Ujerumani juzi Jumatano kiliwachengua mashabiki wake kwa onyesho lililofanyika ndani ya jumba la ajabu la "Klimahaus  Arena” mjini Bremerhaven, Ujerumani, ambapo uwanja wa dansi ulionekana mdogo.
Ngoma Africa Band aka  maarufu kwa majina mengi ya utani kama vile "Watoto wa Mbwa" au "Wazee wa Bongo Tambarare" watatumbuiza tena siku ya Jumamosi hii katika Maonyesho ya AFRIKA-MESSE mijini Bremen, Ujerumani.
Usikose kuwasikiliza at www.ngoma-africa.com

No comments:

Post a Comment