Saturday, December 29, 2012

BABY MADAHA: SIPO TAYARI KUZAA


Na Mwandishi wetu
STAA wa filamu na muziki Bongo, Baby Joseph Madaha amefunguka kuwa hayupo tayari kuzaa kwa sasa.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Baby Madaha aliweka wazi kuwa yupo bize sana na kazi zake za muziki na filamu hivyo suala la kunyonyesha litampotezea muda wake.

“We ubebe mimba sasa hivi, uilee halafu uje kunyonyesha, haya madili ya mjini yote yatafanywa na nani?” alihoji Baby Madaha na kuongeza:
“Mikakati yangu kwa mwaka 2013 ni kuhakikisha nafanya mapinduzi makubwa katika muziki wa Bongo Fleva na filamu.”

No comments:

Post a Comment