Monday, February 25, 2013

PETER AMANDUS ASHINDA TSHS 5,000,000 ZA DSTV REWARDS‏


 Peter Amandus mfanyakazi wa TRA (kati) akifurahia Tshs 5,000,000 alipozawadiwa na DStv kwa kulipia akaunti yake ya DStv kabla ya kukatika. Kulia ni Barbara Kambogi (Meneja Uhusiano), Ronald Shelukindo (Meneja Uendeshaji) na Furaha Samalu (Meneja Masoko) wa kampuni ya MultiChoice Tanzania.
Tunafurahi kwamba tumepata mshindi wetu wa kwanza wa DStv Rewards, bwana Peter Amandus, ambaye ni mshindi wa Tshs 5,000,000.
Mwaka huu DStv kwa kuridhishwa na ushirikiano mkubwa inayopata kutoka kwa wateja wake imeaanda kampeni mpya iitwayo DStv Rewards. Kampeni hii itakuwa inazawadia wateja wake Shilingi za Tanzania 5,000,000 kila wiki endapo mteja atalipia malipo ya mwezi kabla akaunti yake haijakatika.
Mpango huu umekuja miezi michache tu baada ya DStv kuzindua kampeni ya punguzo ya malipo ya mwezi kwa asilimia kumi (10%) kwa vifurushi vyake vyote. Hii ni kama moja ya zawadi zake kwa wateja endepo mteja atalipia  malipo ya mwezi kabla akaunti yake haijakatika.
Nitatuma picha muda si mrefu.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali usisite kuwasiliana nami.

No comments:

Post a Comment