Wednesday, January 1, 2014

Mwombeki aeleza alivyofuatwa na Yanga


Mshambuliaji wa Simba, Betram Mwombeki. 
Na Lucy Mgina
MSHAMBULIAJI wa Simba, Betram Mwombeki, amesema ilibaki kidogo atue Yanga, lakini viongozi wa Simba walishitukia ishu hiyo na kuamua kumsainisha haraka.
Mwombeki alijiunga na Simba msimu huu akitokea Pamba ya Mwanza kwa mkataba wa miaka miwili.
Akizungumza na Championi Jumatano, Mwombeki alisema wakati akifanya mazoezi na klabu ya Simba ambayo ilikuwa ikimfanyia majaribio kwanza ndipo Yanga walipomuona na kutaka kumsainisha mkataba.
Alisema Simba walishitukia mapema suala hilo kabla ya kuamua kumpa mkataba haraka hivyo Yanga wakawa wamemkosa.  Timu nyingine ambazo zilikuwa zikimwania mshambuliaji huyo ni Coastal Union, JKT Ruvu na Ruvu Shooting.   
Hata hivyo, Mwombeki ambaye ni mrefu na mwenye umbo kubwa alisema kwa sasa hayupo tayari kuichezea Yanga na endapo ataondoka Simba hatojiunga na mabingwa hao watetezi wa ligi kuu msimu uliopita.
“Yanga walinifuata wakati  nafanya mazoezi Simba kipindi hicho hata Simba walikuwa bado hawajanipa mkataba na waliposhitukia ishu hiyo ndipo wakanisainisha haraka.
“Kama Simba wangechelewa nigeweza kutua Jangwani,”  alisema Mwombeki.

No comments:

Post a Comment