Siku moja baada ya kuwa baba, Lionel Messi
alitumaini kuwa angefunga bao katika mechi dhidi ya Celta Vigo kwa
ajili kumzawadia mwanae.
Japokuwa Barca waliendeleza rekodi yao ya
kutofungwa katika mechi 10 na ushindi wa 3-, Messi aliyeonekana kuwa
mchovu na mwenye kutaka kufunga hakuweza kutimiza lengo lake baada ya
kutokuwemo kwenye orodha ya wafungaji.
Inawezekana ni uchovu wa kumshughulikia
mtoto wake na demu wake kwa siku mbili kabla ya mechi au kutokuwa katika
siku nzuri uwanjani, Messi alishindwa kufunga na hili lilionekana
kumkera hasa pale mchezaji wa Celta Vigo Jonathan Vilma alipoingilia na
kulivunja shambulizi la Messi kuelekea golini - Messi alijibu mapigo kwa
kurusha ngumi dhaifu kwenye mgongo wa Vilma. Hili lilipelekea kutokea
kwa purukushani baina ya wachezaji wa Celta Vigo na mchezaji huyo bora
wa dunia.

chanzo: shaffih dauda blog
No comments:
Post a Comment