Saturday, March 30, 2013

KILICHOMUUA MBUNGE WA CUF NI HIKI

Na.Mwandishi Wetu
Kilichosababisha kifo cha Mbunge wa Chambani kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Salum Hemed Khamis (pichani), ni maradhi ya moyo na matumizi ya dawa za shinikizo la damu bila kufuata utaratibu, imefahamika.
Kwa mujibu wa taarifa ya daktari aliyeomba hifadhi ya jina lake gazetini, Khamis, alitumia dawa za kudhibiti shinikizo la damu bila kula na wakati huohuo, alifanya kazi mfululizo bila kuchoka
“Ni hatari sana kutumia dawa za presha bila kula. Ni lazima kupumzika, mtu anayetumia dawa za presha anatakiwa awe analala kwa muda mrefu, sasa yule mheshimiwa alikuwa kwenye kipindi kigumu cha kuumwa, akaendelea kufanya kazi halafu kula hakuzingatia,” alisema daktari huyo, anayetoa huduma kwenye Hospitali ya Taifa, Muhimbili.
Khamis, alianguka ghafla Jumatano ya wiki hii akiwa ofisi ndogo za Bunge, Dar es Salaam akiwa kwenye shughuli za kamati za bunge, hivyo kukimbizwa Hospitali ya Taifa, Muhimbili kwa matibabu.
Alifariki dunia juzi (Alhamisi) wakati madaktari wa Muhimbili wakiendelea kumpa matibabu ya kuokoa uhai wake.
Sisi wote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake lazima tutarejea.

No comments:

Post a Comment