Wednesday, April 3, 2013

WASHINDI ZAIDI WA PROMOSHENI YA VODACOM MAHELA WAZIDI KUPATIKANA


Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha nchini, Abdallah Hemedy, akionesha moja ya namba ya simu ya mshindi wa Promosheni ya "MAHELA" aliyejishindia kitita cha shilingi milioni moja, katikati ni Meneja wa huduma za ziada wa Vodacom Tanzania, Bw. Benjamin Michael na  Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Bw. Matina Nkurlu. 
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Bw. Matina Nkurlu, akiongea kwenye simu na mmoja wa washindi aliyejishindia shilingi milioni moja  katika  Promosheni ya "MAHELA" inayoendeshwa na kampuni hiyo, wanaoshuhudia katikati ni Meneja wa huduma za ziada wa kampuni hiyo, Bw. Benjamin Michael, na Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha nchini, Abdallah Hemedy. Zaidi ya shilingi milioni 152 bado zinaendelea kushindaniwa, mteja anatakiwa kutuma neno MAHELA kwenda namba 15544 ili aweze kujinyakulia fedha taslimu.

No comments:

Post a Comment